5 Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi--ila amewahuzunisha ninyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi.
6 Adhabu aliyokwisha pata kutoka kwa wengi wenu inamtosha.
7 Iliyobakia ni afadhali kwenu kumsamehe mtu huyo na kumpa moyo ili asije akahuzunika mno na kukata tamaa kabisa.
8 Kwa hiyo nawasihi: mwonyesheni kwamba mnampenda.