15 Kisha malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, "Sasa utawala juu ya ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Naye atatawala milele na milele!"