11 Naja kwako upesi! Linda, basi, ulicho nacho sasa, ili usije ukanyanganywa na mtu yeyote taji yako ya ushindi.
12 "Wale wanaoshinda nitawafanya wawe minara katika Hekalu la Mungu wangu, na hawatatoka humo kamwe. Pia nitaandika juu yao jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, yaani Yerusalemu mpya, mji ambao utashuka kutoka juu mbinguni kwa Mungu wangu. Tena nitaandika juu yao jina langu jipya.