1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema.
2 "Waheshimu Baba na mama yako," hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani,
3 "Upate fanaka na miaka mingi duniani."
4 Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.