27 Nawaambieni kweli, kuna wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu."
28 Yapata siku nane baada ya kusema hayo, Yesu aliwachukua Petro, Yohane na Yakobo, akaenda nao mlimani kusali.
29 Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa meupe na kungaa sana.
30 Na watu wawili wakaonekana wakizungumza naye, nao ni Mose na Eliya,
31 ambao walitokea wakiwa wenye utukufu, wakazungumza naye juu ya kifo chake ambacho angekikamilisha huko Yerusalemu.