16 Muwe na wema uleule kwa kila mtu. Msijitakie makuu, bali jishugulisheni na watu wadogo. Msijione kuwa wenye hekima sana.
12 Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke.
16 Vitu vyote vya ulimwengu-tamaa mbaya za mwili, vitu wanavyoviona watu na kuvitamani, majivuno yasababishwayo na mali-vyote hivyo havitoki kwa Baba, bali vyatoka kwa ulimwengu.
17 Lakini kama yasemavyo Maandiko: "Mwenye kuona fahari na aone fahari juu ya alichofanya Bwana."
18 Anayekubaliwa si yule anayejisifu mwenyewe, bali yule anayesifiwa na Bwana.
3 Nikitoa mali yangu yote na kuwapa maskini, na tena nikiutoa mwili wangu uchomwe, kama sina upendo hiyo hainifai chochote.
5 Kadhalika nanyi vijana mnapaswa kujiweka chini ya mamlaka ya wazee. Ninyi nyote mnapaswa kuwa na unyenyekevu mpate kutumikiana; maana Maandiko Matakatifu yasema: "Mungu huwapinga wenye majivuno, lakini huwajalia neema wanyenyekevu."
6 Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa enzi wa Mungu, ili awainue wakati ufaao.
7 Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.
9 Ndugu aliye maskini anapaswa kufurahi wakati Mungu anapomkweza,
10 naye tajiri anapaswa kufurahi anaposhushwa na Mungu. Maana tajiri atatoweka kama ua la porini.
17 Waamuru watu walio matajiri katika mambo ya maisha ya sasa, wasijivune, wasiweke tumaini lao katika mali isiyoweza kutegemewa; bali wamtegemee Mungu, ambaye kwa ukarimu hutupatia vitu vyote tuvifurahie.
11 Kwa maana yeyote anayejikweza atashushwa, na anayejishusha, atakwezwa."
20 Akaendelea kusema, "Kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia najisi.
21 Kwa maana kutoka ndani, katika moyo wa mtu, hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji,
22 uzinzi, uchoyo, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, kashfa, kiburi na upumbavu.
23 Maovu hayo yote yatoka ndani ya mtu, nayo humtia mtu najisi."
6 Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko: "Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu."
10 Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni.
22 Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni mapendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu,
23 upole na kuwa na kiasi. Hakuna Sheria inayoweza kupinga mambo hayo.
28 Mungu ameyachagua yale ambayo kwa fikira za dunia ni mambo yaliyo duni na yanayodharauliwa, mambo ambayo hata hayakuwako, ili kwa hayo ayafutilie mbali yale ambayo kwa fikira za binadamu ni mambo ya maana.
29 Basi, hakuna mtu awezaye kujivunia chochote mbele ya Mungu.