4 Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.
1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema.
2 "Waheshimu Baba na mama yako," hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani,
3 "Upate fanaka na miaka mingi duniani."
21 Nanyi wazazi, msiwachukize watoto wenu, la sivyo watakata tamaa.
11 Mtoto akimwomba baba yake samaki, je, atampa nyoka badala ya samaki?
12 Na kama akimwomba yai, je, atampa nge?
13 Ninyi, ingawa ni waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri. Basi, baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho Mtakatifu wale wanaomwomba."
8 Lakini kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani kwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini.
4 Lakini mjane aliye na watoto au wajukuu, hao wanapaswa kujifunza kutimiza wajibu wao wa kidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyo kuwalipa wazazi wao na wazee wao, kwani hilo ni jambo la kupendeza mbele ya Mungu.
7 Vumilieni adhabu kwani ni mafundisho; Mungu huwatendea ninyi kama wanawe. Maana ni mwana gani asiyeadhibiwa na baba yake?
20 Enyi watoto, watiini wazazi wenu daima maana hiyo humpendeza Bwana.