2 Lakini anayeingia kwa kupitia mlangoni, huyo ndiye mchungaji wa kondoo.
3 Mngoja mlango wa zizi humfungulia, na kondoo husikia sauti yake, naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwa jina lake na kuwaongoza nje.
4 Akisha watoa nje huwatangulia mbele nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.
25 Ninyi mlikuwa kama kondoo waliokuwa wamepotea; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mlinzi wa roho zenu.
11 "Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake.
4 Na wakati Mchungaji Mkuu atakapotokea, ninyi mtapokea taji ya utukufu isiyofifia.
14 Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi,
15 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao.
16 Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.