12 Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha stahimili atapewa tuzo la uzima ambalo Mungu aliwaahidia wale wanaompenda.
13 Kama mtu akijaribiwa, asiseme: "Ninajaribiwa na Mungu." Maana Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, wala yeye hamjaribu mtu yeyote.
14 Lakini mtu hujaribiwa anapovutwa na kunaswa na tamaa zake mbaya.
15 Tamaa ikiiva huzaa dhambi; nayo dhambi ikikomaa huzaa kifo.