13 Basi, sasa sikilizeni ninyi mnaosema: "Leo au kesho tutakwenda katika mji fulani na kukaa huko mwaka mzima tukifanya biashara na kupata faida."
14 Ninyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Ninyi ni kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena.
15 Mngalipaswa kusema: "Bwana akitujalia tutaishi na tutafanya hiki au kile."
16 Lakini sasa mwajivuna na kujigamba; majivuno ya namna hiyo ni mabaya.
17 Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa kulifanya, anatenda dhambi.
publicidade